Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Televisheni ya al Alam imelinukuu gazeti hilo likiripoti hayo na kuongeza kuwa, maafisa wa Marekani na Saudia wamesema kuwa, akiba ya silaha za Saudi Arabia imepungua vibaya mno na kwa sura hatari. Hayo yamekuja huku kukiwa na taarifa kwamba viongozi wa Marekani wamekaribia kuafiki rasmi kuipa silaha mpya Saudia za kuwashambulia wananchi wa Yemen.
Gazeti la Wall Street Jouranal la nchini Marekani limeongeza kuwa, kupungua vibaya silaha za Saudia hasa makombora ya patriot ya kukabiliana na makombora na ndege zisizo na rubani za jeshi la Yemen na Ansarullah, kumewatia wahka mkubwa viongozi wa Saudia.
Viongozi wa Riyadh wanaogopa kushambuliwa maeneo nyeti na muhimu sana ya nchi hiyo kama shambulio la mwezi Januari mwaka huu dhidi ya majengo ya ofisi ya kifalme na wasiweze kukabiliana na mashambulio hayo.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa, licha ya kuweko malalamiko makubwa ndani ya Marekani kutokana na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu na masuala mengine nchini Saudi Arabia, lakini viongozi wa Marekani wanaona hawana njia nyingine isipokuwa kuisaidia nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta hasa kutokana na kuwa, baada ya bei ya mafuta kupanda duniani, Washington inaogopa kutokea mashambulio makubwa katika taasisi za mafuta za Saudia na kupelekea kupanda zaidi bei ya mafuta katika soko la dunia.
Gazeti hilo la Marekani limekumbusha pia kuwa, Saudia imeiomba Qatar na nchi za Ulaya kuipa mamia ya makombora ya patriot kwa ajili ya kukabiliana na mashambulio ya Ansarullah na jeshi la Yemen.
342/